An-Nahl 16:27
النحلثُمَّ يَوْمَ ٱلْقِيَـٰمَةِ يُخْزِيهِمْ وَيَقُولُ أَيْنَ شُرَكَآءِىَ ٱلَّذِينَ كُنتُمْ تُشَـٰٓقُّونَ فِيهِمْ ۚ قَالَ ٱلَّذِينَ أُوتُوا۟ ٱلْعِلْمَ إِنَّ ٱلْخِزْىَ ٱلْيَوْمَ وَٱلسُّوٓءَ عَلَى ٱلْكَـٰفِرِينَ
Kisha Siku ya Kiyama atawahizi na atasema: Wako wapi hao washirika wangu ambao kwao mlikuwa mkipinga (Manabii)? Watasema wale waliopewa elimu: Hakika leo ndiyo hizaya na ubaya vitawashukia makafiri.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Kisha Siku ya Kiyama atawahizi na atasema: Wako wapi hao washirika wangu ambao kwao mkiwakutisha (Manabii) mashaka? Watasema walio pewa ilimu:Hakika leo ndiyo hizaya na adhabu itawashukia makafiri, [27]
[27] Na kisha huko Akhera watapo fufuliwa watu na wakahisabiwa kwa vitendo vyao, Mwenyezi Mungu atawasimamisha msimamo wa hizaya na fedheha, atapo wafedhehi na afichue waliyo kuwa wakiyaficha vifuani mwao. Atawaambia: Wako wapi hao miungu mliyo ifanya kuwa ni washirika wangu kwa kuwaabudu? Nanyi kwa ajili yao mlikuwa mkinipiga vita Mimi na Mitume wangu! Wako wapi wapate kukuungeni mkono, kama mlivyo kuwa mkidai? Hawatoweza kujibu! Na hapo tena wale wanao ijua Haki, miongoni mwa Manabii, na Waumini, na Malaika, watasema: Leo ndiyo hizaya na adhabu mbaya kabisa zitawashukia makafiri!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Kisha Siku ya Kiyama Allah Mtukufu Atawafedhehi na Atawafanya wanyonge kwa adhabu na Atasema, «Wako wapi washirika wangu miongoni mwa waungu mliowaabudu badala yangu ili wawatetee msipate adhabu, na hali mlikuwa mkiwapiga vita Manabii na Waumini na mkiwafanyia uadui kwa sababu ya waungu hao?» Wanavyuoni wachamungu watasema, «Hakika udhalili na adhabu ndani ya Siku hii zitawashukia wenye kumkanusha Allah Mtukufu na Mitume Wake».
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net