Ruka hadi kwenye maudhui
Tafsir As-Saadi - Swahili · An-Nahl
Sura ya 16

An-Nahl

Hii ni tarjama ya tafsiri ya as-Saʿdī kama IslamHouse.com inavyoichapisha katika saadi.islamenc.com, iliyosomwa kutoka kurasa za tovuti hiyo. Tovuti haisemi ni nani aliyeitafsiri kwa lugha nyingine wala inafuata toleo gani lililochapishwa, na haitaji masharti ya kuchukua matini yake, kwa hiyo haki ya kuionyesha haijathibitishwa. Hakuna aliyeilinganisha na kitabu kilichochapishwa, na hakuna mwanazuoni aliyeihakiki. Kila kifungu kipo kando ya aya inazozifafanua, ambazo ni matini ya Qur’ani ya Tanzil, inavyoonekana huko; aya ambayo tovuti haitoi ufafanuzi wake yenyewe inakaa pamoja na kifungu kilichotangulia, na faharasa inataja kila aya ya aina hiyo. Sabīl haikuandika wala kutafsiri kwa lugha nyingine chochote kati yake.

Maandishi kutokasaadi.islamenc.comIslamHouse.comnone stated (the site names no licence and no terms for taking its text)ilichukuliwa 2026-10-22

Aya ya 33

هَلْ يَنظُرُونَ إِلَّآ أَن تَأْتِيَهُمُ ٱلْمَلَـٰٓئِكَةُ أَوْ يَأْتِىَ أَمْرُ رَبِّكَ ۚ كَذَٰلِكَ فَعَلَ ٱلَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ ۚ وَمَا ظَلَمَهُمُ ٱللَّهُ وَلَـٰكِن كَانُوٓا۟ أَنفُسَهُمْ يَظْلِمُونَ 33

{33} Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema: Je, wanangojea hawa ambao wamefikiwa na ishara lakini hawakuamini, na wakakumbushwa, lakini hawakukumbuka, "isipokuwa Malaika wawafikie" ili kuchukua roho zao, "au iwafikie amri ya Mola wako Mlezi" ya adhabu itakayowapata? Kwa maana, hakika wameshastahili kufikiwa nayo. "Kama hivyo, walitenda wale waliokuwa kabla yao" walikadhibisha na wakakufuru, kisha hawakuamini mpaka adhabu ilipowateremkia. "Na Mwenyezi Mungu hakuwadhulumu" alipowaadhibu, "lakini walijidhulumu wenyewe." Kwa maana hizo ziliumbwa ili kumwabudu Mwenyezi Mungu, ili yawe maishio yao ni katika utukufu wa Mwenyezi Mungu, lakini wakazidhulumu na wakaacha kile ziliumbwa kwa ajili yake, na wakaziweka katika uduni wa kudumu na taabu isiyoisha.