Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 16 · Aya ya 21

An-Nahl 16:21

النحل

أَمْوَٰتٌ غَيْرُ أَحْيَآءٍ ۖ وَمَا يَشْعُرُونَ أَيَّانَ يُبْعَثُونَ

Maana

Ni wafu, si wahai, na wala hawajui watafufuliwa lini.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Ni wafu si wahai, na wala hawajui watafufuliwa lini. [21]

[21] Na hayo ni vitu visivyo na roho kama maiti, hayana hisiya yoyote, wala hayataharaki, wala hayajui Kiyama kitakuja lini, wala lini watafufuliwa hao wanao yaabudu. Wala si laiki yenu, enyi wenye akili, baada ya haya mkadhani kuwa yatakufaeni kitu hata mkayashirikisha na Mwenyezi Mungu katika kuyaabudu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Wote hao ni visiki, havina uhai, wala hawajui wakati ambao Allah Mtukufu Atawafufua wale wanaowaabudu. Na waungu hao pamoja na wanaowaabudu wote watatupwa Motoni Siku ya Kiyama.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nahl

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net