Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 16 · Aya ya 20

An-Nahl 16:20

النحل

وَٱلَّذِينَ يَدْعُونَ مِن دُونِ ٱللَّهِ لَا يَخْلُقُونَ شَيْـًٔا وَهُمْ يُخْلَقُونَ

Maana

Na wale wanaowaomba wasiokuwa Mwenyezi Mungu hawaumbi kitu, bali wao wameumbwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wale wanao waomba wasio kuwa Mwenyezi Mungu hawaumbi kitu,bali wao wameumbwa. [20]

[20] Huyu Muumba, na Mjuzi wa kila kitu, ndiye Yeye peke yake anaye stahiki kuabudiwa. Ama hayo masanamu mnayo yaabudu, hayo hayawezi kuumba chochote, hata nzi. Bali hayo yenyewe yameumbwa, na pengine mmeyaunda nyinyi wenyewe kwa mikono yenu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na wale waungu ambao washirikina wanawaabudu hawaumbi chochote hata kama ni kidogo vipi. Hao ni viumbe ambavyo washirikina wamevitengeneza kwa mikono yao. Vipi basi wataviabudu?

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nahl

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net