An-Nahl 16:22
النحلإِلَـٰهُكُمْ إِلَـٰهٌ وَٰحِدٌ ۚ فَٱلَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِٱلْـَٔاخِرَةِ قُلُوبُهُم مُّنكِرَةٌ وَهُم مُّسْتَكْبِرُونَ
Mungu wenu ni Mungu Mmoja. Lakini wale wasioiamini Akhera nyoyo zao zinakataa, nao wanatakabari.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Mungu wenu ni Mungu Mmoja. Lakini wasio iamini Akhera nyoyo zao zinakataa, nao wanajivuna. [22]
[22] Na imekwisha wekwa wazi kwa kila dalili kwamba hakika Mungu wenu anaye pasa mumuabudu peke yake ni Mungu Mmoja ambaye hana mshirika wake. Na juu ya hayo wale wasio amini kufufuliwa na kuhisabiwa, nyoyo zao zinaukataa Upweke wake. Kiburi chao kinawazuia kufuata Haki na kuit'ii.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Mola wenu Ndiye Mstahiki wa kuabudiwa Peke Yake. Yeye Ndiye Allah Mtukufu Mmoja Peke Yake, hivyo basi wale wasioamini kufufuliwa, nyoyo zao ni zenye kuukanusha upweke Wake, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, kwa kutoogopa mateso Yake. Kwa hivyo, wao wana ujeuri wa kutoikubali haki na kukataa kumuabudu Allah Mtukufu Peke Yake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net