Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 16 · Aya ya 18

An-Nahl 16:18

النحل

وَإِن تَعُدُّوا۟ نِعْمَةَ ٱللَّهِ لَا تُحْصُوهَآ ۗ إِنَّ ٱللَّهَ لَغَفُورٌ رَّحِيمٌ

Maana

Na mkizihesabu neema za Mwenyezi Mungu, hamwezi kuzidhibiti. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye maghfira mno, Mwingi wa kurehemu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na mkizihisabu neema za Mwenyezi Mungu, hamwezi kuzidhibiti.Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye maghfira, Mwenye kurehemu. [18]

[18] Na mkitaka kuzihisabu neema za Mwenyezi Mungu juu yenu, hamwezi kuzidhibiti. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe, Mkunjufu wa rehema. Basi tubuni kwake, na mumsafie ibada, ili apate kukusameheni na kukurehemuni.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na mkijaribu kuzidhibiti neema za Allah Mtukufu kwenu, ili mjue idadi yake, hamuwezi kuzidhibiti kwa wingi wake na utafauti wake. Hakika Allah Mtukufu ni Mwingi wa kusamehe, ni Mwenye huruma kwenu, kwani Anasamehe kasoro zenu za kutotekeleza ushukuru wa neema, wala Hazikati kwenu, kwa kukiuka kwenu mipaka, wala Hawaharakishii mateso.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nahl

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net