An-Nahl 16:17
النحلأَفَمَن يَخْلُقُ كَمَن لَّا يَخْلُقُ ۗ أَفَلَا تَذَكَّرُونَ
Ati yule anayeumba ni kama asiyeumba? Basi hebu hamkumbuki?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Ati anaye umba ni kama asiye umba? Basi hebu, hamkumbuki? [17]
[17] Hebu ni sawa kwa mwenye akili nzima baina ya Muweza na asiye weza, hata akamfanya Mwenye kuumba yote haya sawa na asiye weza kuumba kitu? Enyi washirikina! Hivyo hamzioni athari za uwezo wa Mwenyezi Mungu mkazingatia na mkamshukuru kwazo Mwenyezi Mungu?
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Basi mnamfanya Allah Mtukufu Ambaye Anaviumba vitu hivi na vinginevyo, katika kustahiki Kwake kuabudiwa Peke Yake, ni kama waungu wanaodhaniwa ambao hawaumbi chochote? Basi hamkumbuki utukufu wa Allah Mtukufu mkamuabudu Yeye Peke Yake?
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net