An-Nahl 16:125
النحلٱدْعُ إِلَىٰ سَبِيلِ رَبِّكَ بِٱلْحِكْمَةِ وَٱلْمَوْعِظَةِ ٱلْحَسَنَةِ ۖ وَجَـٰدِلْهُم بِٱلَّتِى هِىَ أَحْسَنُ ۚ إِنَّ رَبَّكَ هُوَ أَعْلَمُ بِمَن ضَلَّ عَن سَبِيلِهِۦ ۖ وَهُوَ أَعْلَمُ بِٱلْمُهْتَدِينَ
Lingania kwenye njia ya Mola wako Mlezi kwa hekima na mawaidha mazuri, na ujadiliane nao kwa namna iliyo nzuri zaidi. Hakika Mola wako Mlezi ndiye anayemjua zaidi yule aliyeipotea njia yake, na Yeye ndiye anayewajua zaidi wale walioongoka.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Waite waelekee kwenye Njia ya Mola wako Mlezi kwa hikima na mawaidha mema, na ujadiliane nao kwa namna iliyo bora. Hakika Mola wako Mlezi ndiye anaye mjua zaidi aliye ipotea Njia yake, na Yeye ndiye anaye wajua zaidi walio ongoka. [125]
[125] Ewe Nabii! Lingania, uwite watu kwenye Njia ya Haki ambayo Mola wako Mlezi amewataka watu wako waifuate. Na katika huo Wito wako pita njia ambayo inamnasibu kila mmoja wao. Waite wenye vyeo vya juu katika wao kwa maneno ya hikima kwa mujibu wa akili zao. Na watu wa kawaida walio baki kati yao walinganie kwa kuwapa mawaidha yanao waelekea, na kuwapigia mifano ya mambo wanayo pambana nayo ya kuwapeleka kwenye Haki, na uwaongoze kwenye njia fupi inayo wanasibu. Na jadiliana na watu wa dini zilizo tangulia katika watu wa Biblia, yaani Mayahudi na Wakristo, kwa kutumia hoja za kiakili, Mant'iqi, na maneno laini, na majadiliano mazuri, si maneno ya ukali na matusi, ili uwakinaishe na uwavutie. Hii ndiyo njia ya Daa'wa (Wito), kuwaita watu kumwendea Mwenyezi Mungu -watu wa mila zote. Basi ifuate njia hii unapo waita, na baada ya hayo yaliyo baki mwachilie Mola wako Mlezi, ambaye anamjua aliye zama katika upotovu kati yao na akawa mbali na njia ya uwokovu, na nani ambaye aliye salimika, akaongoka, na akayaamini hayo uliyo waletea.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Lingania, ewe Mtume, wewe na aliyekufuata, kwenye Dini ya Mola wako na njia Yake iliyonyooka kwa kutumia hekima ambayo Allah Mtukufu alikuletea wahyi nayo ndani ya Qur’ani na Sunnah. Na uwazungumzie watu kwa njia inayolingana na wao, uwape nasaha kwa njia nzuri yenye kuwavutia kwenye kheri na kuwahimiza wajiepushe na shari, na ujadiliane na wao kwa njia nzuri za kujadiliana za utaratibu na upole, kwani si juu yako isipokuwa kufikisha ujumbe, na ushafikisha. Ama kuwafanya waongoke, hilo ni juu ya Allah Mtukufu Peke Yake. Yeye Ndiye Anayemjua zaidi yule aliyepotea na akaiyepuka njia Yake, na Yeye Anawajua zaidi walioongoka.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net