Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 16 · Aya ya 126

An-Nahl 16:126

النحل

وَإِنْ عَاقَبْتُمْ فَعَاقِبُوا۟ بِمِثْلِ مَا عُوقِبْتُم بِهِۦ ۖ وَلَئِن صَبَرْتُمْ لَهُوَ خَيْرٌ لِّلصَّـٰبِرِينَ

Maana

Na mkilipiza, basi lipizeni sawa na vile mlivyoadhibiwa. Na ikiwa mtasubiri, basi hakika hivyo ni bora zaidi kwa wanaosubiri.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na mkilipiza basi lipizeni sawa na vile mlivyo adhibiwa. Na ikiwa mtasubiri, basi hakika hivyo ni bora zaidi kwa wanao subiri. [126]

[126] Enyi Waislamu! Mkitaka kuwaadhibu wale wanao kufanyieni uadui wakakuvamieni, basi waadhibuni kwa kadiri walivyo kutendeeni, wala msizidishe kuliko hivyo. Na kuweni na yakini kwamba mkistahamili, msijilipizie kisasi, itakuwa ni kheri zaidi kwenu hapa duniani na Akhera. Basi toeni adhabu kwa ajili ya Haki, wala msiadhibu kwa ajili ya nafsi zenu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na mkitaka kuwalipizia kisasi, enyi Waumini, wale waliowafanyia uadui, msiongeze zaidi ya vile walivyowafanya. Na mkisubiri, basi hilo ni bora kwenu nyinyi ulimwenguni, kwa kupewa ushindi, na kesho Akhera, kwa kupewa malipo makubwa.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nahl

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net