An-Nahl 16:124
النحلإِنَّمَا جُعِلَ ٱلسَّبْتُ عَلَى ٱلَّذِينَ ٱخْتَلَفُوا۟ فِيهِ ۚ وَإِنَّ رَبَّكَ لَيَحْكُمُ بَيْنَهُمْ يَوْمَ ٱلْقِيَـٰمَةِ فِيمَا كَانُوا۟ فِيهِ يَخْتَلِفُونَ
Hakika siku ya Sabato (Jumamosi) waliwekewa wale waliohitilafiana kuhusiana nayo. Na hakika Mola wako Mlezi bila ya shaka atahukumu baina yao Siku ya Kiyama katika yale waliyokuwa wakihitilafiana.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hakika siku ya Sabato (Jumaamosi) waliwekewa wale walio khitalifiana kwa ajili yake. Na hakika Mola wako Mlezi bila ya shaka atahukumu baina yao Siku ya Kiyama katika yale waliyo kuwa wakikhitalifiana. [124]
[124] Wala sio kuitukuza siku ya Ijumaa na kuiacha Jumaamosi kama ilivyo katika Uislamu kuwa ni kukhitalifiana na alivyo kuwa akifanya Ibrahim, kama wanavyo dai Mayahudi. Kwani kuharimishwa kuvua (na kufanya kazi nyengine) siku ya Jumaamosi, ndio Siku ya Sabato, kwa sababu ya kuitukuza haikuwamo katika sharia ya Ibrahim. Hayo walilazimishwa Mayahudi tu (ambao hata hawakuwapo zama za Ibrahim). Na juu ya hivyo hawakuitukuza, bali baadhi yao waliacha kutukuza huko, na wakenda kinyume na amri ya Mola wao Mlezi. Basi yawaje hata wanawatia makosani wengine kwa kutolazimishwa kutukuza jambo ambalo wao walio lazimishwa wameliasi? Ewe Nabii! Kuwa na yakini kuwa Mola wako Mlezi atawahukumu hao Siku ya Kiyama katika hayo mambo wanayo khitalifiana kwayo, na atamlipa kila mmoja wao kwa vitendo vyake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Allah Mtukufu Ameufanya utukuzaji wa siku ya Jumamosi, kwa kuitenga kwa kufanya ibada ndani yake, kwa Mayahudi ambao walitafautiana na Nabii wao juu yake, na wakaiteua badala ya siku ya Ijumaa ambayo waliamrishwa waitukuze. Hakika Mola wako, ewe Mtume, ni Mwenye kuhukumu baina ya wale waliotafautiana na Nabii wao Siku ya Kiyama na kumlipa kila mmoja kwa yale anayofaa kuyapata.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net