Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 16 · Aya ya 123

An-Nahl 16:123

النحل

ثُمَّ أَوْحَيْنَآ إِلَيْكَ أَنِ ٱتَّبِعْ مِلَّةَ إِبْرَٰهِيمَ حَنِيفًا ۖ وَمَا كَانَ مِنَ ٱلْمُشْرِكِينَ

Maana

Kisha tukakufunulia ya kwamba ufuate mila ya Ibrahim, mnyoofu kwa Mwenyezi Mungu, wala hakuwa miongoni mwa washirikina.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Kisha tukakufunulia ya kwamba ufuate mila ya Ibrahim, mwongofu,wala hakuwa miongoni mwa washirikina. [123]

[123] Ewe Nabii! Baada ya Ibrahim kwa karne nyingi, tulikupa Wahyi wewe, na tukakuamrisha umfuate Ibrahim katika wito wake wa kulingania Tawhid, na fadhila njema, na kujiepusha na dini za uwongo. Kwani yeye hakuwa katika wanao mshirikisha Mwenyezi Mungu, kama wanavyo msingizia hawa washirikina.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kisha tukakuletea wahyi, ewe Mtume, kwamba uifuate dini ya Uislamu kama alivyoifuata Ibrãhîm na kwamba unyooke juu yake na usiende kinyume nayo, kwani Ibrãhîm hakuwa ni miongoni mwa wale wanaomshirikisha Allah pamoja na viumbe.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nahl

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net