An-Nahl 16:120
النحلإِنَّ إِبْرَٰهِيمَ كَانَ أُمَّةً قَانِتًا لِّلَّهِ حَنِيفًا وَلَمْ يَكُ مِنَ ٱلْمُشْرِكِينَ
Hakika Ibrahim alikuwa mfano mwema, mnyenyekevu kwa Mwenyezi Mungu, mnyoofu kwa Mwenyezi Mungu, wala hakuwa miongoni mwa washirikina.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hakika Ibrahim alikuwa mfano mwema, mnyenyekevu kwa MwenyeziMungu, mwongofu, wala hakuwa miongoni mwa washirikina. [120]
[120] Hakika Ibrahim, mnaye tafakhari naye nyinyi washirikina na Mayahudi, alikuwa amekusanya kila fadhila njema, na yu mbali na upotovu wenu, ni mt'iifu wa amri ya Mola wake Mlezi, na wala hakuwa mshirikina kama nyinyi.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakika Ibrãhîm alikuwa kiongozi katika mema, na alikuwa mtiifu mnyenyekevu kwa Allah Mtukufu, haendi kombo na Uislamu, ni mwenye kumpwekesha Allah Mtukufu, si mwenye kumshirikisha.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net