An-Nahl 16:121
النحلشَاكِرًا لِّأَنْعُمِهِ ۚ ٱجْتَبَىٰهُ وَهَدَىٰهُ إِلَىٰ صِرَٰطٍ مُّسْتَقِيمٍ
Mwenye kuzishukuru neema zake. Yeye alimteua, na akamwongoa kwenye njia iliyonyooka.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Mwenye kuzishukuru neema zake, Mwenyezi Mungu. Yeye kamteuwa,na akamwongoa kwenye Njia Iliyo Nyooka. [121]
[121] Alikuwa mwenye kushukuru kwa neema za Mola wake Mlezi. Na kwa haya yote ndio Mwenyezi Mungu alimteua ili abebe Ujumbe wake, na akamwezesha kufuata Njia ya Haki Iliyo Nyooka yenye kufikilia kwenye neema ya kudumu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na alikuwa ni mwenye kuzishukuru neema za Allah Mtukufu kwake. Allah Mtukufu Alimchagua kwa ujumbe Wake na Akamuongoza kwenye njia iliyonyooka, nayo ni Uislamu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net