An-Nahl 16:119
النحلثُمَّ إِنَّ رَبَّكَ لِلَّذِينَ عَمِلُوا۟ ٱلسُّوٓءَ بِجَهَـٰلَةٍ ثُمَّ تَابُوا۟ مِنۢ بَعْدِ ذَٰلِكَ وَأَصْلَحُوٓا۟ إِنَّ رَبَّكَ مِنۢ بَعْدِهَا لَغَفُورٌ رَّحِيمٌ
Kisha hakika Mola wako Mlezi kwa wale waliotenda mabaya kwa ujinga, kisha wakatubia baada ya hayo na wakatenda mazuri; bila ya shaka Mola wako Mlezi baada ya hayo ni Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa kurehemu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Kisha hakika Mola wako Mlezi kwa walio tenda uovu kwa ujinga,kisha wakatubia baada ya hayo na wakatenda mema; bila ya shaka Mola wako Mlezi baada ya hayo ni Mwenye kusamehe na Mwenye kurehemu. [119]
[119] Kisha wanao tenda maovu kwa kupitikiwa, au kwa kuacha kuzingatia vilivyo matokeo yatayo tokea, na baadae wakatubia, wakajitengeneza nafsi zao na vitendo vyao, basi hakika Mola wako Mlezi, ewe Nabii, atawasamehe hao madhambi yao. Kwani hakika Yeye Subhanahu baada ya toba hiyo ni Mwingi wa kusamehe madhambi, na ni Mkunjufu wa rehema kwa waja wake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Kisha hakika Mola wako, kwa wale waliofanya maasia, kwa kutojua mwisho wake na kwamba yanasababisha kupata hasira za Allah Mtukufu -kwani kila anayemuasi Allah Mtukufu, kwa kukosea au kwa kusudia, huwa ni mjinga kwa mtazamo huu, hata kama anajua kuwa ni haramu-, kisha wakarudi kwa Allah Mtukufu na kuyaacha yale madhambi waliokuwa wakiyafanya na wakazitengeneza nafsi zao na matendo yao, hakika Mola wako, baada ya kutubia kwao na kutengenea kwao, ni Mwenye kuwasamehe, ni Mwenye huruma kwao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net