An-Nahl 16:118
النحلوَعَلَى ٱلَّذِينَ هَادُوا۟ حَرَّمْنَا مَا قَصَصْنَا عَلَيْكَ مِن قَبْلُ ۖ وَمَا ظَلَمْنَـٰهُمْ وَلَـٰكِن كَانُوٓا۟ أَنفُسَهُمْ يَظْلِمُونَ
Na Mayahudi tuliwaharimishia yale tuliyokuhadithia zamani. Na Sisi hatukuwadhulumu, bali walikuwa wakijudhulumu wenyewe.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na Mayahudi tuliwaharimishia yale tuliyo kuhadithia zamani.Na Sisi hatukuwadhulumu, bali walikuwa wakijudhulumu wenyewe. [118]
[118] Wala hawakuharimishiwa ila Mayahudi tu vile vitu tulivyo kusimulia, ewe Nabii, kabla ya kuteremka Aya hizi. Na vitu hivyo ni kuwa kila mnyama mwenye makucha, na shahamu za ng'ombe na kondoo, ila ilio beba migongo yao au matumbo, au iliyo changanyika na mifupa. Na Sisi hatukuwadhulumu kwa kuwaharimishia hayo, lakini wamejidhulumu wenyewe kuyasabibisha hayo kwa kupita mipaka na ushari wao, na kuacha kusimama kwenye yalio halali...
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na Mayahudi tuliwaharamishia vile vitu tulivyokupa habari zake, ewe Mtume, kabla, navyo ni kila mnyama mwenye kucha na mafuta ya ng’ombe, mbuzi na kondoo, isipokuwa kile kilichobebwa na migongo yao au matumbo yao au kilichotangamana na mifupa. Na sisi hatukuwadhulumu wao, lakini wao walikuwa ni wenye kuzidhulumu nafsi zao kwa kukanusha na kufanya uadui, ndipo wakastahili kuharamishiwa kwa njia ya kutiwa adabu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net