An-Nahl 16:115
النحلإِنَّمَا حَرَّمَ عَلَيْكُمُ ٱلْمَيْتَةَ وَٱلدَّمَ وَلَحْمَ ٱلْخِنزِيرِ وَمَآ أُهِلَّ لِغَيْرِ ٱللَّهِ بِهِۦ ۖ فَمَنِ ٱضْطُرَّ غَيْرَ بَاغٍ وَلَا عَادٍ فَإِنَّ ٱللَّهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ
Hakika amewaharimishia tu nyamafu, na damu, na nyama ya nguruwe, na mnyama aliyechinjwa kwa ajili ya asiyekuwa Mwenyezi Mungu. Lakini anayelazimishwa bila ya kuasi, wala kuvuka mipaka, basi hakika Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa kurehemu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Amekuharimishieni nyamafu tu, na damu, na nyama ya nguruwe,na mnyama aliye chinjwa kwa ajili isiyo kuwa ya Mwenyezi Mungu. Lakini anaye lazimishwa bila ya kuasi, wala kuruka mipaka, basi hakika MwenyeziMungu ni Mwenye kusamehe na Mwenye kurehemu. [115]
[115] Kwani hakika Mwenyezi Mungu hakukuharimishieni isipo kuwa nyamafu, na damu inayo tiririka kutokana na mnyama wakati wa kumchinja, na nyama ya nguruwe, na kilicho chinjwa kwa asiye kuwa Mwenyezi Mungu. Lakini mwenye kulazimishwa na shida ya njaa kula kitu alicho kuharimishieni Mwenyezi Mungu, bila ya kutaka, na wala bila ya kupita hadi ya kiasi cha kuondoa ile dharura, basi hakika Mwenyezi Mungu hayachukulii hayo. Kwani Yeye Subhanahu ni Mwenye kuwasamehe waja wake. Huwasamehe wanapo tumbukia katika makosa wasio endelea nayo. Naye ni Mwenye kuwarehemu kwa vile anawazuia vitu vinavyo wadhuru, na anawaruhusu kwa kuhifadhi uhai wao.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakika Amewaharamishia mfu wa mnyama, damu yenye kutiririka kutoka kwa mnyama aliechinjwa pale achinjwapo, nyama ya nguruwe na mnyama aliyechinjiwa asiyekuwa Allah Mtukufu. Lakini yoyote Aliyelazimika kula chochote kati ya vitu hivi vilivyoharamishwa, kwa dharura ya kuogopa kufa, na hali yeye si dhalimu wala si mkiukaji mpaka wa dharura, basi Allah Mtukufu ni Mwenye kumsamehe na ni Mwenye huruma naye, Hatamuadhibu kwa kitendo alichokifanya.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net