Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 16 · Aya ya 114

An-Nahl 16:114

النحل

فَكُلُوا۟ مِمَّا رَزَقَكُمُ ٱللَّهُ حَلَـٰلًا طَيِّبًا وَٱشْكُرُوا۟ نِعْمَتَ ٱللَّهِ إِن كُنتُمْ إِيَّاهُ تَعْبُدُونَ

Maana

Basi kuleni katika vile alivyowaruzuku Mwenyezi Mungu, vilivyo halali na vizuri. Na shukuruni neema za Mwenyezi Mungu, ikiwa kweli mnamuabudu Yeye tu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Basi kuleni katika vile alivyo kupeni Mwenyezi Mungu, vilivyo halali na vizuri. Na shukuruni neema za Mwenyezi Mungu, ikiwa kweli mnamuabudu Yeye. [114]

[114] Ikiwa washirikina wanazikufuru neema za Mwenyezi Mungu na wanazigeuza kuwa ni nakama, basi nyinyi Waumini elekeeni kwenye shukra. Na kuleni katika alivyo kuruzukuni Mwenyezi Mungu na akakufanyieni kuwa ni vizuri kwenu, wala msijiharimishie nafsi zenu. Na ishukuruni neema ya Mwenyezi Mungu iliyo juu yenu kwa kumt'ii Yeye tu peke yake, ikiwa kweli mnamkusudia Yeye tu kwa ibada.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Basi kuleni, enyi Waumini, miongoni mwa vile ambavyo Allah Mtukufu Amewaruzuku na Akavifanya ni halali nzuri kwenu. Na shukuruni neema za Allah Mtukufu kwenu, kwa kuzitambua na kuzitumia katika kumtii Allah Mtukufu, iwapo nyinyi, ni wenye kufuata amri Yake, ni wenye kusikia na kumtii Yeye, mnamuabudu Yeye Peke Yake, Asiye na mshirika.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nahl

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net