An-Nahl 16:113
النحلوَلَقَدْ جَآءَهُمْ رَسُولٌ مِّنْهُمْ فَكَذَّبُوهُ فَأَخَذَهُمُ ٱلْعَذَابُ وَهُمْ ظَـٰلِمُونَ
Na alikwishawajia Mjumbe kutoka miongoni mwao. Lakini wakamkadhibisha; basi ikawachukua adhabu hali ya kuwa ni madhalimu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na alikwisha wajia Mjumbe wa miongoni mwao wenyewe. Lakini wakamkanusha;basi iliwafika adhabu hali ya kuwa wamedhulumu. [113]
[113] Nao alikwisha wajia Mtume kutokana nao wenyewe. Ilikuwa ni waajibu wao wamshukuru Mwenyezi Mungu kwa hayo, lakini walimwambia mwongo, kwa inda na husda tu. Adhabu ikawatwaa nao hali wamo katika udhalimu, na kwa sababu ya hiyo dhulma.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hakika Allah Mtukufu Alipeleka kwa watu wa Makkah Mtume miongoni mwao, yeye ni Nabii Muhammad, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), wanaijua nasaba yake, ukweli wake na uaminifu wake, wakayakataa yale aliyowajia nayo na hawakuamini. Hapo iliwapata adhabu ya shida, njaa, hofu na kuuawa wakuu wao huko Badr na hali wao ni madhalimu wa nafsi zao kwa kumshirikisha Allah Mtukufu na kuwazuia watu na njia Yake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net