Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 16 · Aya ya 112

An-Nahl 16:112

النحل

وَضَرَبَ ٱللَّهُ مَثَلًا قَرْيَةً كَانَتْ ءَامِنَةً مُّطْمَئِنَّةً يَأْتِيهَا رِزْقُهَا رَغَدًا مِّن كُلِّ مَكَانٍ فَكَفَرَتْ بِأَنْعُمِ ٱللَّهِ فَأَذَٰقَهَا ٱللَّهُ لِبَاسَ ٱلْجُوعِ وَٱلْخَوْفِ بِمَا كَانُوا۟ يَصْنَعُونَ

Maana

Na Mwenyezi Mungu amepiga mfano wa mji uliokuwa na amani na utulivu, riziki yake ikiufikia kwa wingi kutokea kila mahali. Lakini ukazikufuru neema za Mwenyezi Mungu; kwa hivyo Mwenyezi Mungu akauvisha vazi la njaa na hofu kwa sababu ya yale waliyokuwa wakiyafanya.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na Mwenyezi Mungu amepiga mfano wa mji ulio kuwa na amani na utulivu, riziki yake ikiufikia kwa nafasi kutoka kila mahali. Lakini ukazikufuru neema za Mwenyezi Mungu; kwa hivyo Mwenyezi Mungu akauvika vazi la njaa na khofu kwa sababu ya yale waliyo kuwa wakiyafanya. [112]

[112] Na Mwenyezi Mungu Subhanahu amewapigia mfano watu wa Makka kisa cha mji mmojapo. Watu wake walikuwa wamekaa kwa amani, hawana adui anaye waingilia. Wametua, hawana dhiki ya maisha, riziki inawajia kwa wasaa kutoka kila pahali. Wakazibeua neema za Mwenyezi Mungu, wasimshukuru kwa kumt'ii na kutekeleza amri zake. Mwenyezi Mungu akawapatiliza kwa masaibu yaliyo wazunguka kila upande. Wakaonja uchungu wa njaa na vitisho, baada ya utajiri na amani walio kuwa nayo. Na hayo kwa sababu ya kukakamia kwao katika ukafiri na maasi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na Allah Mtukufu Amepiga mfano wa mji wa Makkah. Ulikuwa uko kwenye salama ya kutofanyiwa uadui, na utulivu usio na dhiki za maisha, na unajiliwa na riziki zake kwa uzuri na usahali kutoka kila upande, wakazi wake wakazikanusha neema za Allah Mtukufu kwao, wakamshirikisha na wasimshukuru, hapo Allah Mtukufu akawaadhibu kwa njaa na hofu kwa kuviogopa vikosi vya Mtume, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), na majeshi yake yaliyokuwa yakiwatisha, na hili ni kwa sababu ya ukafiri wao na vitendo vyao vya ubatilifu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nahl

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net