Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 16 · Aya ya 111

An-Nahl 16:111

النحل

يَوْمَ تَأْتِى كُلُّ نَفْسٍ تُجَـٰدِلُ عَن نَّفْسِهَا وَتُوَفَّىٰ كُلُّ نَفْسٍ مَّا عَمِلَتْ وَهُمْ لَا يُظْلَمُونَ

Maana

Siku ambayo kila nafsi itakuja ikijitetea, na kila nafsi italipwa kikamilifu yale iliyotenda, nao hawatadhulumiwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Siku ambayo kila nafsi itakuja jitetea, na kila nafsi italipwa sawa sawa na a'mali ilizo zifanya, nao hawatadhulumiwa. [111]

[111] Ewe Nabii! Watajie watu wako, kwa kuwahadharisha, Siku ambayo kila mtu atakuwa hana linalo mshughulisha ila kujitetea nafsi yake. Hayamshughulishi ya mzazi wala mwana. Siku hiyo ndiyo Siku ya Kiyama! Na Mwenyezi Mungu siku hiyo atailipa kila nafsi malipo ya vitendo iliyo tenda, ikiwa kheri au shari. Na Mola wako Mlezi hamdhulumu hata mtu mmoja.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na wakumbushe wao, ewe Mtume, Siku ya Kiyama pindi itakapokuja kila nafsi ikijitetea yenyewe na kutoa nyudhuru za kila aina, na hapo Allah Mtukufu Ailipe kila nafsi malipo ya ilichokifanya bila ya kuidhulumu. Hatawaongezea mateso wala hawatapunguziwa malipo yao.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nahl

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net