An-Nahl 16:110
النحلثُمَّ إِنَّ رَبَّكَ لِلَّذِينَ هَاجَرُوا۟ مِنۢ بَعْدِ مَا فُتِنُوا۟ ثُمَّ جَـٰهَدُوا۟ وَصَبَرُوٓا۟ إِنَّ رَبَّكَ مِنۢ بَعْدِهَا لَغَفُورٌ رَّحِيمٌ
Kisha hakika Mola wako Mlezi, kwa wale waliohama makwao baada ya kuteswa, kisha wakapigania Dini na wakasubiri, bila ya shaka Mola wako Mlezi baada ya hayo ni Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa kurehemu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Kisha hakika Mola wako Mlezi, kwa wale walio hama makwao baada ya kuteswa, kisha wakapigania Dini na wakasubiri, bila ya shaka Mola wako Mlezi baada ya hayo ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu. [110]
[110] Tena, ewe Nabii! Jua kuwa Mola wako Mlezi ni Mwenye kuwasaidia na kuwanusuru walio hama Makka kukimbiza Dini yao isikandamizwe, na nafsi zao zisiadhibiwe na washirikina. Kisha wakapigana Jihadi kwa kadiri ya uwezo wao, kwa maneno na vitendo, wakavumilia mashaka na taabu, na yaliyo wakuta kwa ajili ya Dini yao. Hakika Mola wako Mlezi baada ya hayo waliyo yastahamilia ni Mwenye kuwasamehe wakitubu, Mwenye kuwarehemu, basi hato wachukulia kwa walio lazimishwa kuyafanya.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Kisha Mola wako, kwa wale waliofanywa wanyonge ndani ya Makkah na wakaadhibiwa na washirikina mpaka wakakubali matendo yao kijuujuu, wakawafitini kwa kutamka yanayowaridhi, na hali nyoyo zao zimetulia katika Imani, na ilipowezekana kwao kujiokoa wakahama kwenda Madina kisha wakapigana jihadi katika njia ya Allah Mtukufu na wakavumilia mashaka ya majukumu, hakika Mola wako, baada ya kutubia kwao ni Mwenye kuwasamehe, ni Mwenye kuwarehemu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net