An-Nahl 16:116
النحلوَلَا تَقُولُوا۟ لِمَا تَصِفُ أَلْسِنَتُكُمُ ٱلْكَذِبَ هَـٰذَا حَلَـٰلٌ وَهَـٰذَا حَرَامٌ لِّتَفْتَرُوا۟ عَلَى ٱللَّهِ ٱلْكَذِبَ ۚ إِنَّ ٱلَّذِينَ يَفْتَرُونَ عَلَى ٱللَّهِ ٱلْكَذِبَ لَا يُفْلِحُونَ
Wala msiseme uongo, kwa kuropokwa na ndimi zenu: Hiki ni halali, na hiki ni haramu - mkimzulia uongo Mwenyezi Mungu. Hakika wale wanaomzulia uongo Mwenyezi Mungu hawatafaulu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wala msiseme uwongo, kwa kuropokwa na ndimi zenu: Hichi halali,na hichi haramu - mkimzulia uwongo Mwenyezi Mungu. Hakika wanao mzulia uwongo Mwenyezi Mungu hawatafanikiwa. [116]
[116] Na ilivyo kuwa Mwenyezi Mungu amekwisha kubainishieni kilicho halali na kilicho haramu, basi shikamaneni na hayo aliyo kubainishieni, wala msithubutu kuhalalisha na kuharimisha ovyo kufuata ndimi zenu. Mkawa mnasema: Hichi halali, na hichi haramu. Matokeo ya hizo kauli zenu ni kumzulia uwongo Mwenyezi Mungu, na kumkhusisha na asiyo yasema! Hakika wanao mzulia uwongo Mwenyezi Mungu hawapati kheri wala mafanikio.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Wala msiseme, enyi washirikina, urongo unaotolewa na ndimi zenu: «hii ni halali» juu ya kitu kilichoharamishwa «na hii ni haramu» juu ya kitu kilichohalalishwa, ili kumzulia Allah Mtukufu urongo kwa kumnasibishia uhalalishaji na uharamishaji. Hakika wale wanaomzulia Allah Mtukufu urongo hawatafaulu kupata wema wowote ulimwenguni wala Akhera.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net