Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 16 · Aya ya 107

An-Nahl 16:107

النحل

ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمُ ٱسْتَحَبُّوا۟ ٱلْحَيَوٰةَ ٱلدُّنْيَا عَلَى ٱلْـَٔاخِرَةِ وَأَنَّ ٱللَّهَ لَا يَهْدِى ٱلْقَوْمَ ٱلْكَـٰفِرِينَ

Maana

Hayo ni kwa sababu wameupendelea uhai wa dunia hii kuliko Akhera, na kwa sababu Mwenyezi Mungu hawaongoi kaumu makafiri.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Hayo ni kwa sababu wameyapenda zaidi maisha ya duniani kuliko ya Akhera, na kwa sababu Mwenyezi Mungu hawaongoi watu makafiri. [107]

[107] Na hiyo ghadhabu na adhabu waliyo stahiki kuipata, ni kwa sababu ya kupenda kwao mno neema za duniani na starehe zake za kupita njia, hata zikawaweka mbali na Haki, na zikawatia upofu wasiione kheri. Basi Mwenyezi Mungu akawaachilia mbali na huo ukafiri wanao upenda. Huo ndio mwendo wake anavyo watendea viumbe vyake, huwaacha kama hawa, na huwaacha asiwahidi kwa sababu ya ufisadi wao wenyewe, na kukakamia katika upotovu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hiyo ni kwa sababu ya kuchagua kwao dunia na pambo lake na kuifanya kwao hiyo dunia kuwa ni bora kuliko Akhera na malipo yake na kwamba Allah Mtukufu Hawaongozi makafiri wala hawaelekezi kwenye haki na usawa.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nahl

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net