Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 16 · Aya ya 106

An-Nahl 16:106

النحل

مَن كَفَرَ بِٱللَّهِ مِنۢ بَعْدِ إِيمَـٰنِهِۦٓ إِلَّا مَنْ أُكْرِهَ وَقَلْبُهُۥ مُطْمَئِنٌّۢ بِٱلْإِيمَـٰنِ وَلَـٰكِن مَّن شَرَحَ بِٱلْكُفْرِ صَدْرًا فَعَلَيْهِمْ غَضَبٌ مِّنَ ٱللَّهِ وَلَهُمْ عَذَابٌ عَظِيمٌ

Maana

Anayemkufuru Mwenyezi Mungu baada ya kuamini kwake - isipokuwa yule aliyelazimishwa na hali ya kuwa moyo wake umetua juu ya Imani, lakini yule aliyekifungulia kifua chake ukafiri - basi hao ghadhabu ya Mwenyezi Mungu ipo juu yao, na wao wana adhabu kubwa.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Anaye mkataa Mwenyezi Mungu baada ya kuamini kwake - isipo kuwa aliye lazimishwa na hali ya kuwa moyo wake umetua juu ya Imani, lakini aliye kifungulia kifua chake kukataa - basi hao ghadhabu ya Mwenyezi Mungu ipo juu yao, na wao watapata adhabu kubwa. [106]

[106] Hao wanao tamka ukafiri baada ya kuamini watapata ghadhabu ya Mwenyezi Mungu. Isipo kuwa aliye lazimishwa kutamka maneno ya ukafiri na hali moyo wake umesimama imara katika Imani. Huyo atavuka, haitompata ghadhabu ya Mwenyezi Mungu. Ama ambao nyoyo zao zinafurahia ukafiri, na ndimi zao zinakubaliana na yaliyo nyoyoni mwao, hao watapata ghadhabu kali kwa Mwenyezi Mungu ambaye amewaandalia adhabu kubwa katika Akhera.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Hakika wanaozua urongo ni wanaotamka neno la ukafiri na kuritadi baada ya kuamini. Hao itawashukia wao hasira kutoka kwa Allah Mtukufu, isipokuwa yule aliyelazimishwa kutamka maneno ya ukafiri na akayatamka kwa kuchelea kuangamia, hali moyo wake umejikita kwenye Imani, basi huyo hana lawama. Lakini mwenye kutamka ukafiri na moyo wake ukatulia juu yake, hao watashukiwa na hasira kali kutoka kwa Allah Mtukufu na watapata adhabu kubwa.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

An-Nahl

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net