An-Nahl 16:105
النحلإِنَّمَا يَفْتَرِى ٱلْكَذِبَ ٱلَّذِينَ لَا يُؤْمِنُونَ بِـَٔايَـٰتِ ٱللَّهِ ۖ وَأُو۟لَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلْكَـٰذِبُونَ
Hakika wanazua uongo tu wale wasioziamini Ishara za Mwenyezi Mungu. Na hao ndio waongo.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Wanao zua uwongo ni wale tu wasio ziamini Ishara za MwenyeziMungu. Na hao ndio waongo. [105]
[105] Hakika wanao jasirisha kumzulia Mwenyezi Mungu uwongo ni wale wasio ziamini Ishara za Mwenyezi Mungu, na hao peke yao ndio walio fikilia ukomo wa uwongo. Na wewe, Nabii, si katika watu hao hata wa kutuhumie hivyo.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Kwa hakika wanaozua urongo ni wale wasiomuamini Allah Mtukufu na aya Zake, na wao ndio warongo kwa neno lao hilo. Ama Muhammad, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie, anayemuamini Mola wake na kumnyenyekea, haiwezekani kwake yeye kumkanusha Allah Mtukufu na kumsingizia Asiyoyasema.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net