An-Nahl 16:108
النحلأُو۟لَـٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ طَبَعَ ٱللَّهُ عَلَىٰ قُلُوبِهِمْ وَسَمْعِهِمْ وَأَبْصَـٰرِهِمْ ۖ وَأُو۟لَـٰٓئِكَ هُمُ ٱلْغَـٰفِلُونَ
Hao ndio ambao Mwenyezi Mungu ameziziba nyoyo zao na kusikia kwao na kuona kwao. Na hao ndio walioghafilika.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hao ndio Mwenyezi Mungu ameziziba nyoyo zao na masikio yao na macho yao. Na hao ndio walio ghafilika. [108]
[108] Hao ndio Mwenyezi Mungu amewapiga muhuri wa mghafala katika nyoyo zao, hata zikawa haziikubali Haki, na katika masikio yao wakawa hawasikii kwa sikio la fahamu na mazingatio wakawa kama viziwi, na katika macho yao hata wakawa hawaoni ishara na dalili zilio mbele yao. Hao ndio walio zama katika kughafilika na Haki. Hao hawana kheri mpaka uondoke mghafala katika akili zao.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hao ndio wale ambao Allah Mtukufu Amewapiga muhuri nyoyo zao kwa ukafiri na ufadhilishaji dunia juu ya Akhera, hazitafikiwa na nuru ya uongofu, na Amewafanya viziwi masikio yao kutozisikia aya za Allah Mtukufu, kusikia kwa kuzingatia, na Amewafanya vipofu macho yao wasizione hoja zinazojulisha uungu wa Allah Mtukufu, na hao ndio wenye kughafilika na ile adhabu Aliyowaandalia Allah Mtukufu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net