Ibrahim 14:28
ابراهيمأَلَمْ تَرَ إِلَى ٱلَّذِينَ بَدَّلُوا۟ نِعْمَتَ ٱللَّهِ كُفْرًا وَأَحَلُّوا۟ قَوْمَهُمْ دَارَ ٱلْبَوَارِ
Je, hukuwaona wale waliobadilisha neema ya Mwenyezi Mungu kwa kufuru, na wakawafikisha kaumu yao kwenye nyumba ya maangamizo?
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hebu hukuwaona wale walio badilisha neema ya Mwenyezi Mungu kwa kufuru, na wakawafikisha watu wao kwenye nyumba ya maangamizo? [28]
[28] Ewe msikilizaji! Hebu huwaangalii hao washirikina ambao, badala ya kushukuru neema ya Mwenyezi Mungu ya kumleta Muhammad na Dini yake, wakaingia kumkataa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na wakawasabibisha wafwasi wao kutumbukia katika nyumba ya hilaki kwa upotovu wao.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Kwani hutazami, ewe mwenye kuambiwa (makusudio ni jumla ya wenye kuambiwa), hali ya wakanushaji miongoni mwa makafiri wa Kikureshi waliochagua kumkanusha Allah Mtukufu badala ya kumshukuru kwa neema ya amani na kutumilizwa Nabii Muhammad, rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie, kwao wao? Na kwa hakika waliwashukisha wafuasi wao nyumba ya maangamivu, waliposababisha kuwatoa wao kwenda Badr wakauawa, na mwisho wao ukawa ni nyumba ya maangamivu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net