Ibrahim 14:29
ابراهيمجَهَنَّمَ يَصْلَوْنَهَا ۖ وَبِئْسَ ٱلْقَرَارُ
Nayo ni Jahannamu wataiingia! Na ni mahali pa kukaa pabaya mno!
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Nayo ni Jahannamu! Wataingia, Maovu yaliyoje makaazi hayo! [29]
[29] Na nyumba hiyo ndiyo Jahannamu wakiteswa kwa uvukuto wake. Na makaazi maovu mno ni Jahannamu.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
nayo ni Moto wa Jahanamu ambao watauingia na wataungua na joto lake. Na mahali pabaya pa kukaa na kutulia ni hapo penye makao yao.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net