Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 14 · Aya ya 27

Ibrahim 14:27

ابراهيم

يُثَبِّتُ ٱللَّهُ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ بِٱلْقَوْلِ ٱلثَّابِتِ فِى ٱلْحَيَوٰةِ ٱلدُّنْيَا وَفِى ٱلْـَٔاخِرَةِ ۖ وَيُضِلُّ ٱللَّهُ ٱلظَّـٰلِمِينَ ۚ وَيَفْعَلُ ٱللَّهُ مَا يَشَآءُ

Maana

Mwenyezi Mungu huwaimarisha wale walioamini kwa kauli ya imara katika uhai wa dunia na katika Akhera. Na Mwenyezi Mungu huwapoteza madhalimu. Na Mwenyezi Mungu hufanya apendavyo.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Mwenyezi Mungu huwatia imara wenye kuamini kwa kauli ya imara katika maisha ya dunia na katika Akhera. Na Mwenyezi Mungu huwaacha kupotea hao wenye kudhulumu. Na Mwenyezi Mungu hufanya apendavyo. [27]

[27] Mwenyezi Mungu anawathibitisha imara wanao amini juu ya neno la Haki katika uhai wa duniani na Siku ya Kiyama pia. Na Mwenyezi Mungu huwabaidisha nalo neno hilo makafiri kwa kutojitengenezea wenyewe. Mwenyezi Mungu hutenda atakavyo, akiwathibitisha baadhi na kuwaacha kupotea wenginewe. Hapana wa kumtoa kombo kwa hukumu yake, wala mwenye kuurudisha uamuzi wake!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Allah Mtukufu Anawathibitisha wale walioamini kwenye neno la ukweli lenye uimara nalo ni kukubali kwamba hakuna mola anayepasa kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah Mtukufu na kwamba Muhammad ni Mtume wa Allah Mtukufu, kwamba Atawathibitisha kwenye dini ya kweli aliyokuja nayo katika huu ulimwengu, Atawapa mwisho mwema wakati wa kufa, na Atawaongoza watoe jawabu ya sawa watakapoulizwa na Malaika wawili kaburini. Na Allah Mtukufu Atawapoteza madhalimu wasiuone usawa ulimwenguni na Akhera. Na Allah Mtukufu Anafanya Analolitaka kwa kuwapa taufiq wenye kuamini na kutowaongoza wenye kukufuru na kuasi.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Ibrahim

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net