Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 14 · Aya ya 26

Ibrahim 14:26

ابراهيم

وَمَثَلُ كَلِمَةٍ خَبِيثَةٍ كَشَجَرَةٍ خَبِيثَةٍ ٱجْتُثَّتْ مِن فَوْقِ ٱلْأَرْضِ مَا لَهَا مِن قَرَارٍ

Maana

Na mfano wa neno ovu ni kama mti muovu, uliong'olewa juu ya ardhi. Hauna uimara wowote.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na mfano wa neno ovu ni kama mti muovu, ulio ng'olewa juu ya ardhi. Hauna imara. [26]

[26] Neno la uwongo baya mfano wake ni kama mti mbaya ulio ng'olewa, umetupwa juu ya ardhi. Haukusimama imara. Hali kadhaalika neno la uwongo lilio kataliwa halina uthabiti, kwa kuwa halikuungwa mkono na hoja.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na mfano wa neno ovu, nalo ni neno la ukafiri, ni kama mti muovu wa chakula na ladha, nao ni mti wa subili, uliong’olewa juu ya ardhi, kwa kuwa mizizi yake iko karibu na uso wa ardhi, hauna mizizi iliyojikita ndani wala hauna matawi yenye kwenda juu. Hivyo ndivyo kafiri alivyo, hana uthabiti wala hana wema na wala hakuna tendo jema lake lolote litakalopaishwa kwa Allah Mtukufu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Ibrahim

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net