Ibrahim 14:25
ابراهيمتُؤْتِىٓ أُكُلَهَا كُلَّ حِينٍۭ بِإِذْنِ رَبِّهَا ۗ وَيَضْرِبُ ٱللَّهُ ٱلْأَمْثَالَ لِلنَّاسِ لَعَلَّهُمْ يَتَذَكَّرُونَ
Hutoa matunda yake kila wakati kwa idhini ya Mola wake Mlezi. Na Mwenyezi Mungu huwapigia watu mifano ili wapate kukumbuka.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Hutoa matunda yake kila wakati kwa idhini ya Mola wake Mlezi. Na Mwenyezi Mungu huwapigia watu mifano ili wapate kukumbuka. [25]
[25] Hutoa matunda yake kila wakati aliyo uweka Mwenyezi Mungu yazae kwa mapendekezo ya aliye yaumba. Hivyo hivyo ndio tamshi la Tawhid, Upweke wa Mwenyezi Mungu, ni lenye kuthibiti katika moyo wa Muumini. A'mali yake inapanda kwa Mwenyezi Mungu, na inamfikilia baraka zake na thawabu zake kila wakati. Na Mwenyezi Mungu anawabainishia watu kwa mifano, anashabihisha maana kwa vitu wavijuavyo ili Waumini wawaidhike.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Unatoa matunda yake kila kipindi kwa idhini ya Mola wake. Namna hiyo ndivyo ulivyo mti wa Imani: msingi wake umejikita imara ndani ya moyo wa Muumini kiujuzi na kiitikadi, na matawi yake ya matendo mema na tabia za kuridhisha zinapaishwa juu kwa Allah Mtukufu, na malipo yake mema yanapatikana kila kipindi. Na Allah Mtukufu Anawapigia watu mfano ili wakumbuke na wawaidhike wapate kuzingatia.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net