Ibrahim 14:18
ابراهيممَّثَلُ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ بِرَبِّهِمْ ۖ أَعْمَـٰلُهُمْ كَرَمَادٍ ٱشْتَدَّتْ بِهِ ٱلرِّيحُ فِى يَوْمٍ عَاصِفٍ ۖ لَّا يَقْدِرُونَ مِمَّا كَسَبُوا۟ عَلَىٰ شَىْءٍ ۚ ذَٰلِكَ هُوَ ٱلضَّلَـٰلُ ٱلْبَعِيدُ
Mfano wa wale waliomkufuru Mola wao Mlezi, vitendo vyao ni kama jivu linalopeperushwa kwa nguvu za upepo katika siku ya upepo mkali. Hawawezi kupata chochote katika yale waliyoyachuma. Huko ndiko kupotea kwa mbali!
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Mfano wa walio mkufuru Mola wao Mlezi - vitendo vyao ni kama jivu linalo peperushwa kwa nguvu za upepo katika siku ya mdharba. Hawawezi kupata chochote katika waliyo yafanya. Huko ndiko kupotelea mbali. [18]
[18] Hakika hali za vitendo vya kheri wavifanyavyo makafiri duniani na pato lake, kwa kuwa havikujengwa juu ya msingi wa Imani, hali yake ni kama jivu. Ukaja upepo mkali ukalipeperusha siku ya kimbunga kilipo kaza. Siku ya Kiyama hawapati chochote kutokana na vitendo vyao vya namna hivyo vya duniani. Hayumkini wao kunafiika na chochote kutokana navyo, kwani hivyo havina thawabu, kama mtu mwenye vumbi linalo peperuka katika upepo asilo weza kulikamata. Na watu hawa wapotovu hujiona wenyewe ati kuwa ndio wanafanya mema, na ilhali vitendo vyao viko mbali kabisa na Njia ya Haki.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Hali ya matendo mazuri ya makafiri ulimwenguni, kama vile kufanya wema na kuunga udugu, ni kama hali ya jivu lililopigwa na upepo wa nguvu katika siku yenye upepo mkali usiache hata alama yake. Hivyo ndivyo yatakavyokuwa matendo yao, hawatapata kwa matendo hayo kitu cha kuwanufaisha mbele ya Allah Mtukufu; kwani ukafiri umeyaondoa kama vile upepo ulivyoondoa jivu. Kushughulika huko na kufanya matendo mema huko bila ya msingi, ndio kupotea kuliko mbali na njia ya sawa
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net