Ibrahim 14:19
ابراهيمأَلَمْ تَرَ أَنَّ ٱللَّهَ خَلَقَ ٱلسَّمَـٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضَ بِٱلْحَقِّ ۚ إِن يَشَأْ يُذْهِبْكُمْ وَيَأْتِ بِخَلْقٍ جَدِيدٍ
Je, huoni kuwa Mwenyezi Mungu ameziumba mbingu na ardhi kwa Haki? Akitaka, anawaondoa na alete viumbe wapya!
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Huoni kuwa Mwenyezi Mungu ameziumba mbingu na ardhi kwa Haki? Akitaka atakuondoeni na alete viumbe wapya! [19]
[19] Ewe unae semezwa! Hujui kwamba Mwenyezi Mungu ameziumba mbingu na ardhi zisimame juu ya Haki kwa mujibu wa hikima yake? Na Mwenye kuweza haya basi anaweza kukuteketezeni, enyi makafiri, na akitaka akaleta viumbe wengine badala yenu nyinyi, ambao watakubali kuwepo kwake, na kwamba Yeye ni Mmoja wa pekee.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Je, hujui, ewe mwenye kuambiwa,- na makusudio ni watu kwa jumla- kwamba Allah Mtukufu Ndiye Aliyeumba mbingu na ardhi kwa namna thabiti yenye kuonyesha hekima Yake, na kwamba Yeye Hakuziumba kwa mchezo, bali ni kwa ajili ya kutolea ushahidi juu ya upweke Wake na ukamilifu wa uwezo Wake, ili wamuabudu Peke Yake, na wasimshirikishe na kitu chochote? Basi Akitaka Atawaondoa na Awalete watu wasiokuwa nyinyi wanaomtii Allah Mtukufu.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net