Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 14 · Aya ya 17

Ibrahim 14:17

ابراهيم

يَتَجَرَّعُهُۥ وَلَا يَكَادُ يُسِيغُهُۥ وَيَأْتِيهِ ٱلْمَوْتُ مِن كُلِّ مَكَانٍ وَمَا هُوَ بِمَيِّتٍ ۖ وَمِن وَرَآئِهِۦ عَذَابٌ غَلِيظٌ

Maana

Awe anayagugumiza, wala hataweza kuyameza. Na mauti yatamjia kutokea kila upande, wala hatakufa. Na zaidi ya hayo itakuwepo adhabu nyengine kali.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Awe anayagugumia, wala hawezi kuyameza. Na mauti yawe yanamjia kutoka kila upande, naye wala hafi. Na zaidi ya hayo ipo adhabu nyengine kali vile vile. [17]

[17] Kunywa kwake ni taklifu, ni kama wanayagugumia, na wala hayeshi kiu, kwani hayumkini kuyaonea tamu kwa ukarihi wake na uchafu wake! Na mtu anakuwa ni kama amezungukwa na mauti kila upande kwa shida ziliopo, na wala huko katika Jahannamu hafi akapumzika na yanayo mfika, bali kila wakati anakuta adhabu nyengine kali zaidi.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Mwenye kiburi atajaribu kumeza usaha na damu na vinginevyo vinavyotiririka mara kwa mara kutoka kwa watu wa Motoni, na hataweza kuzimeza kwa uchafu wake, kuunguza kwake na uchungu wake. Na adhabu kali ya kila aina itamjia kwenye kila kiungo katika mwili wake. Hatakuwa ni mwenye kufa akapumzika. Na baada ya adhabu hii atapatiwa adhabu nyingine yenye kuumiza.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Ibrahim

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net