Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 13 · Aya ya 9

Ar-Ra'd 13:9

الرعد

عَـٰلِمُ ٱلْغَيْبِ وَٱلشَّهَـٰدَةِ ٱلْكَبِيرُ ٱلْمُتَعَالِ

Maana

Yeye ndiye Mwenye kujua ya ghaibu na yanayoonekana, Mkubwa, Mtukufu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Yeye ndiye Mwenye kujua yanayo onekana na yasio onekana; Mkuu Aliye tukuka. [9]

[9] Yeye anayajua ya ghaibu tusiyo yahisi, na tunayo yashuhudia kwa ujuzi zaidi kuliko tunavyo shuhudia sisi na kuona. Na Yeye Subhanahu ni Mwenye shani kubwa iliyo tukuka juu ya kila kiumbe.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Allah Mtukufu ni Mjuzi wa yaliyofichika na macho na yanayoonekana, Aliye Mkubwa wa dhati, majina na sifa, Aliye juu ya viumbe Vyake vyote kwa dhati Yake, uwezo Wake na kutendesha nguvu Kwake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Ar-Ra'd

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net