Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 13 · Aya ya 8

Ar-Ra'd 13:8

الرعد

ٱللَّهُ يَعْلَمُ مَا تَحْمِلُ كُلُّ أُنثَىٰ وَمَا تَغِيضُ ٱلْأَرْحَامُ وَمَا تَزْدَادُ ۖ وَكُلُّ شَىْءٍ عِندَهُۥ بِمِقْدَارٍ

Maana

Mwenyezi Mungu anajua mimba ibebwayo na kila cha kike, na kinachopunguka na kuzidi matumboni mwa uzazi. Na kila kitu kwake ni kwa kipimo.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Mwenyezi Mungu anajua mimba abebayo kila mwanamke, na kinacho punguka na kuzidi matumboni. Na kila kitu kwake ni kwa kipimo. [8]

[8] Aliye mpa Mtume huo muujiza mkubwa kabisa ni Yeye anaye jua kila kitu, na anazijua nafsi za binaadamu tangu kuumbwa kwao kutokana na mbegu za uzazi katika tumbo la mama mpaka wakati wa kufa kwao. Basi Yeye anaijua mimba anayo ichukua kila mwanamke kama ni mume au mke, kinacho punguka tumboni na kilicho zidi wakati, mpaka utimie muda wa mimba, na mtoto akamilike kukua, azaliwe. Kila kitu kwake Yeye Subhanahu kina kipimo maalumu, na muda maalumu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Allah Mtukufu Aliyetukuka Anakijua alichokibeba kila mwanamke ndani ya tumbo lake: ni cha kiume au ni cha kike, ni chema au ni kibaya. Na anakijua kile ambacho kizazi kinakipunguza kikazaliwa kimekufa au kabla ya kutimia miezi tisa au kikapita muda huo. Na kila kitu, chenye kuzidi au kupungua, kimekadiriwa kutoka kwa Allah Mtukufu kwa kipimo kisichopitisha kiasi.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Ar-Ra'd

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net