Ar-Ra'd 13:7
الرعدوَيَقُولُ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ لَوْلَآ أُنزِلَ عَلَيْهِ ءَايَةٌ مِّن رَّبِّهِۦٓ ۗ إِنَّمَآ أَنتَ مُنذِرٌ ۖ وَلِكُلِّ قَوْمٍ هَادٍ
Na wale waliokufuru wanasema: Mbona hakuteremshiwa ishara kutoka kwa Mola wake Mlezi? Hakika wewe ni Mwonyaji tu, na kila kaumu ina wa kuwaongoza.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na wale walio kufuru husema: Mbona hakuteremshiwa muujiza kutoka kwa Mola wake Mlezi? Hakika wewe ni Mwonyaji, na kila kaumu ina wa kuwaongoa. [7]
[7] Na husema hao makafiri wasio amini muujiza mkubwa, yaani Qur'ani: Hebu na amteremshie Mola wake Mlezi alama ya unabii wake wa kuonekana kama kuiendesha milima akawa Mwenyezi Mungu anaonyesha wazi uhakika wa Nabii wake katika jambo hili! Na Yeye Subhanahu anamwambia: Hakika wewe ni Nabii wa kuwaonya kwamba kuna adhabu mbaya wakiendelea na upotovu wao. Na kila kaumu wanaye Mtume wa kuwaongoza kwenye Haki, na muujiza wa kubainisha ujumbe wake. Si wao wa kuchagua. Lao ni kujibu upinzani na kuleta mfano wake!
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na makafiri wa Makkah wanasema, «Basi si ajiwe na miujiza inayoonekana kama fimbo ya Mûsã na ngamia wa Sãlih.» Na hilo haliko kwenye mkono wako, ewe Mtume; hukuwa wewe isipokuwa ni mwenye kuwafikishia na ni mwenye Kuwaonya na adhabu ya Allah Mtukufu. Na kila ummah una mjumbe wa kuwaongoza kwenye njia ya Allah Mtukufu Aliyetukuka.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net