Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 13 · Aya ya 6

Ar-Ra'd 13:6

الرعد

وَيَسْتَعْجِلُونَكَ بِٱلسَّيِّئَةِ قَبْلَ ٱلْحَسَنَةِ وَقَدْ خَلَتْ مِن قَبْلِهِمُ ٱلْمَثُلَـٰتُ ۗ وَإِنَّ رَبَّكَ لَذُو مَغْفِرَةٍ لِّلنَّاسِ عَلَىٰ ظُلْمِهِمْ ۖ وَإِنَّ رَبَّكَ لَشَدِيدُ ٱلْعِقَابِ

Maana

Na wanakuharakisha ulete mabaya kabla ya mazuri, hali ya kuwa zimekwishapita kabla yao adhabu za kupigiwa mfano. Na hakika Mola wako Mlezi ni Mwenye msamaha kwa watu juu ya udhalimu wao. Na hakika Mola wako Mlezi ni Mkali wa kuadhibu.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wanakuhimiza ulete maovu kabla ya mema, hali ya kuwa zimekwisha pita kabla yao adhabu za kupigiwa mfano. Na hakika Mola wako Mlezi ni Mwenye msamaha kwa watu juu ya udhalimu wao. Na hakika Mola wako Mlezi ni Mkali wa kuadhibu. [6]

[6] Na huko kupita mpaka upotovu kunawapelekea kutaka wateremshiwa adhabu haraka haraka badala ya kuomba hidaya itayo waokoa. Na wanadhani kwamba Mwenyezi Mungu hawateremshii adhabu duniani akitaka. Na zimekwisha wapitia adhabu watu mfano wao kwa hayo, katika alio wateketeza Mwenyezi Mungu kabla yao. Lakini ni shani ya Mwenyezi Mungu kusamehe dhulma ya mwenye kutubia akarejea kwenye Haki, na kumteremshia adhabu kali anaye endelea na upotovu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na wale wakanushaji wanakuharakisha uwaletee adhabu ambayo mimi sikuwaharakishia kabla ya kuamini Imani ambayo kwayo kunatarajiwa usalama na matendo mema. Na yashapita mateso ya wakanushaji kabla yao, kwa nini wao hawawi ni wenye kuwaidhika na wao? Hakika Mola wako ni Mwenye msamaha wa dhambi za watu waliotubia dhambi zao juu ya udhalimu wao, Atawafungulia mlango wa msamaha na Atawaita waingie, na huku wao wanazidhulumu nafsi zao kwa kumuasi Mola wao. Hakika Mola Wako ni Mkali wa mateso juu ya walioendelea kwenye ukafiri, upotevu na kumuasi Allah Mtukufu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Ar-Ra'd

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net