Ar-Ra'd 13:5
الرعدوَإِن تَعْجَبْ فَعَجَبٌ قَوْلُهُمْ أَءِذَا كُنَّا تُرَٰبًا أَءِنَّا لَفِى خَلْقٍ جَدِيدٍ ۗ أُو۟لَـٰٓئِكَ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ بِرَبِّهِمْ ۖ وَأُو۟لَـٰٓئِكَ ٱلْأَغْلَـٰلُ فِىٓ أَعْنَاقِهِمْ ۖ وَأُو۟لَـٰٓئِكَ أَصْحَـٰبُ ٱلنَّارِ ۖ هُمْ فِيهَا خَـٰلِدُونَ
Na kama ukistaajabu, basi cha ajabu zaidi ni huo usemi wao: Je, tukishakuwa mchanga, kweli tutakuwa katika umbo jipya? Hao ndio waliomkufuru Mola wao Mlezi. Na hao ndio watakaokuwa na makongwa shingoni mwao, na hao ndio watu wa Motoni. Humo watadumu.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na kama ukistaajabu, basi cha ajabu zaidi ni huo usemi wao: Ati tukisha kuwa mchanga kweli tutakuwa katika umbo jipya? Hao ndio walio mkufuru Mola wao Mlezi. Na hao ndio watao kuwa na makongwa shingoni mwao, na hao ndio watu wa Motoni. Humo watadumu. [5]
[5] Na hakika mambo ya washirikina juu ya dalili hizi ni ya ajabu. Ikiwa wewe Muhammad utas- taajabia jambo, basi la ajabu ni hiyo kauli yao wanapo sema: Ati baada ya kufa, na baada ya kwisha kuwa mchanga, tutakuwa wahai tena upya? Huu ndio mtindo wa wanao mkufuru Muumba wao. Akili zao zimefungwa na upotovu. Na marejeo yao ni Motoni watakapo dumu humo; kwani hao ni wenye kukanya juu ya kuwa mwenye kuweza kuanzisha anaweza kurejesha.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Ukiona ajabu, ewe Mtume, ya makafiri kutoamini baada ya dalili hizi, basi ajabu kubwa zaidi ni kusema kwao, «Je, tukifa na tukawa mchanga tutafufuliwa upya?» Hao ndio wenye kumkanusha Mola wao Aliyewafanya waweko kutoka kwenye hali ya kutokuwako. Na hao kutakuwa na minyororo kwenye shingo zao Siku ya Kiyama. Na hao wataingia Motoni na hawatatoka kabisa.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net