Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 13 · Aya ya 10

Ar-Ra'd 13:10

الرعد

سَوَآءٌ مِّنكُم مَّنْ أَسَرَّ ٱلْقَوْلَ وَمَن جَهَرَ بِهِۦ وَمَنْ هُوَ مُسْتَخْفٍۭ بِٱلَّيْلِ وَسَارِبٌۢ بِٱلنَّهَارِ

Maana

Ni sawa anayeficha kauli yake miongoni mwenu na anayeidhihirisha, na anayejibanza usiku na anayetembea jahara mchana.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Ni sawa anaye ficha kauli yake kati yenu na anaye idhihirisha, na anaye jibanza usiku na anaye tembea jahara mchana. [10]

[10] Anazijua hali zenu zote katika maisha yenu, na maneno yenu na vitendo vyenu vyote. Basi anayajua mnayo yaficha na mnayo yatangaza, vitendo na maneno. Na anajua vile mnavyo jificha usiku na kujitokeza mchana. Na yote ni sawa katika ujuzi wake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Analingana, katika ujuzi Wake Aliyetukuka, yule anayefanya usiri katika maneno, katika nyinyi, na anayedhihirisha. Na analingana Kwake yule anayefanya matendo yake kwa siri ndani ya giza la usiku na yule mwenye kuyafanya waziwazi kwenye mwangaza wa mchana.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Ar-Ra'd

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net