Ar-Ra'd 13:11
الرعدلَهُۥ مُعَقِّبَـٰتٌ مِّنۢ بَيْنِ يَدَيْهِ وَمِنْ خَلْفِهِۦ يَحْفَظُونَهُۥ مِنْ أَمْرِ ٱللَّهِ ۗ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يُغَيِّرُ مَا بِقَوْمٍ حَتَّىٰ يُغَيِّرُوا۟ مَا بِأَنفُسِهِمْ ۗ وَإِذَآ أَرَادَ ٱللَّهُ بِقَوْمٍ سُوٓءًا فَلَا مَرَدَّ لَهُۥ ۚ وَمَا لَهُم مِّن دُونِهِۦ مِن وَالٍ
Kila mtu analo kundi la malaika mbele yake na nyuma yake linamlinda kwa amri ya Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu habadilishi yaliyoko kwa kaumu mpaka wabadilishe wao yaliyo katika nafsi zao. Na Mwenyezi Mungu anapowatakia kaumu ubaya, basi hakuna cha kuuzuia wala hawana mlinzi yeyote asiyekuwa Yeye.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Kila mtu analo kundi la malaika mbele yake na nyuma yake linamlinda kwa amri ya Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu habadili yaliyoko kwa watu mpaka wabadili wao yaliyomo naf- sini mwao. Na Mwenyezi Mungu anapo watakia watu adhabu hakuna cha kuzuia wala hawana mlinzi yeyote badala yake. [11]
[11] Na Mwenyezi Mungu Aliye takasika ndiye anaye kuhifadhini. Kila mtu anao Malaika wanao mlinda kwa amri ya Mwenyezi Mungu, na wanapeana zamu kumlinda mbele na nyuma yake. Na hakika Mwenyezi Mungu Subhanahu habadilishi hali ya watu kutoka shida kwendea neema, na kutoka nguvu wakawa dhaifu, mpaka wao wenyewe wageuze waliyo nayo kufuatana na hali wanayo iendea. Na Mwenyezi Mungu akitaka kuwateremshia watu maovu basi hawana wa kuwanusuru ataye walinda na amri yake, wala wa kuwatazamia mambo yao kuwakinga na yatayo wateremkia.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Na Allah Mtukufu aliyetukuka Ana Malaika wanaompitia binadamu, kundi baada ya kundi, mbele yake na nyuma yake, wanamhifadhi kwa amri ya Allah Mtukufu na kuyadhibiti yanayofanywa na yeye, mema au maovu. Hakika Allah Mtukufu, aliyetakasika na kutukuka, Hageuzi neema aliyowaneemesha watu mpaka wakiwa wao watayageuza yale waliyoamrishwa na Mola wao na wakamuasi. Na Allah Mtukufu Akiwatakia watu mitihani basi hakuna namna ya kuikimbia, na hawana wao asiyekuwa Allah Mtukufu msimamizi yoyote wa kuyasimamia mambo yao, akawaletea yanayopendwa na akawakinga na yanayochukiwa.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net