Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 13 · Aya ya 12

Ar-Ra'd 13:12

الرعد

هُوَ ٱلَّذِى يُرِيكُمُ ٱلْبَرْقَ خَوْفًا وَطَمَعًا وَيُنشِئُ ٱلسَّحَابَ ٱلثِّقَالَ

Maana

Yeye ndiye anayewaonyesha umeme kwa hofu na matumaini, na huyaanzisha mawingu mazito.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Yeye ndiye anaye kuonyesheni umeme kwa khofu na tamaa, na huyaleta mawingu mazito. [12]

[12] Na uwezo wa Mwenyezi Mungu Mtukufu katika ulimwengu unaonekana wazi, na athari zake zipo dhaahiri. Ni Yeye anaye kuonesheni umeme, ukakutisheni kuuona au mkakhofu isikujieni mvua wakati msio ihitaji ikakuharibieni mazao, au mkatumai kwa umeme itakuja mvua kubwa mnayo ihitajia kwa maslaha ya ukulima. Ni Yeye anaye yafanya mawingu yaliyo jaa mvua.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Yeye Ndiye Ambaye anawaonesha umeme, nao ni mwangaza unaong’aa kutoka ndani ya mawingu, mkawa mnaogopa msishukiwe na vimondo vyenye kuchoma kutokana na umeme huo, na pia mkawa mnatazamia mvua inyeshe. Na kwa uwezo Wake, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, Anayaleta mawingu yanayobebeshwa maji mengi kwa ajili ya manufaa yenu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Ar-Ra'd

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net