Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 13 · Aya ya 32

Ar-Ra'd 13:32

الرعد

وَلَقَدِ ٱسْتُهْزِئَ بِرُسُلٍ مِّن قَبْلِكَ فَأَمْلَيْتُ لِلَّذِينَ كَفَرُوا۟ ثُمَّ أَخَذْتُهُمْ ۖ فَكَيْفَ كَانَ عِقَابِ

Maana

Na hakika walifanyiwa kejeli Mitume waliokuwa kabla yako. Na nikawapururia wale waliokufuru, kisha nikawashika! Basi ilikuwaje adhabu yangu!

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na hakika walifanyiwa kejeli Mitume walio kuwa kabla yako. Na nikawapururia wale walio kufuru, kisha nikawashika! Basi ilikuwaje adhabu yangu! [32]

[32] Na ikiwa hao wanao kanya wamekufanyia kejeli kwa hayo unao waitia na kwa Qur'ani, basi walifanyiwa maskhara vile vile Mitume walio tumwa kabla yako wewe, ewe Nabii. Basi usihuzunike, kwani mimi nawapa muhula tu hawa wanao kanya, kisha nitawatwaa, na hapo itakuwa adhabu kali isiyo wezekana kuelezwa wala kujuulikana hali yake.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na iwapo wameufanyia shere ulinganizi wako, ewe Mtume, basi kuna ummah kabla yako waliwafanyia shere Mitume wao. Basi usiwe na masikitiko, niliwapa muhula wale waliokufuru kisha nikawapatiliza kwa mateso yangu; na yalikuwa ni mateso makali.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Ar-Ra'd

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net