Ar-Ra'd 13:31
الرعدوَلَوْ أَنَّ قُرْءَانًا سُيِّرَتْ بِهِ ٱلْجِبَالُ أَوْ قُطِّعَتْ بِهِ ٱلْأَرْضُ أَوْ كُلِّمَ بِهِ ٱلْمَوْتَىٰ ۗ بَل لِّلَّهِ ٱلْأَمْرُ جَمِيعًا ۗ أَفَلَمْ يَا۟يْـَٔسِ ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓا۟ أَن لَّوْ يَشَآءُ ٱللَّهُ لَهَدَى ٱلنَّاسَ جَمِيعًا ۗ وَلَا يَزَالُ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ تُصِيبُهُم بِمَا صَنَعُوا۟ قَارِعَةٌ أَوْ تَحُلُّ قَرِيبًا مِّن دَارِهِمْ حَتَّىٰ يَأْتِىَ وَعْدُ ٱللَّهِ ۚ إِنَّ ٱللَّهَ لَا يُخْلِفُ ٱلْمِيعَادَ
Na kama ingelikuwako Qur-ani inayoendeshewa milima, na kupasuliwa kwayo ardhi, na kusemeshwa kwayo wafu, (basi ingelikuwa Qur-ani hii). Bali mambo yote ni ya Mwenyezi Mungu. Je, hawajajua wale walioamini kwamba lau kuwa Mwenyezi Mungu angetaka, bila ya shaka angeliwaongoa watu wote? Na wale waliokufuru hawaachi kusibiwa na balaa kwa yale waliyoyatenda, au ikawateremkia karibu na nyumbani kwao, mpaka ije ahadi ya Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu havunji miadi yake.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na kama ingeli kuwako Qur'ani ndiyo inayo endeshewa milima, na kupasuliwa ardhi, na kusemeshewa wafu, (basi ingeli kuwa Qur'ani hii). Bali mambo yote ni ya Mwenyezi Mungu. Je, hawajajua walio amini kwamba lau kuwa Mwenyezi Mungu ange penda bila ya shaka angeli waongoa watu wote? Wala walio kufuru hawaachi kusibiwa na balaa kwa waliyo yatenda, au ikawateremkia karibu na nyumbani kwao, mpaka ifike ahadi ya Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu havunji miadi yake. [31]
[31] Wao wanataka muujiza mwingine usio kuwa huu wa Qur'ani, juu ya ubora wa athari yake, lau kuwa kweli wanaitaka Haki na wanaikubali. Lau kuwa kuna Kitabu cha kusomwa kikaiendesha milima, kikapasua ardhi, au kikawasemeza maiti, basi Kitabu hicho kinge kuwa hii Qur'ani! Lakini watu hawa wana inda tu. Mwenyezi Mungu peke yake ndiye mwenye amri yote katika miujiza na malipo ya hao wakanyao. Na katika hayo ana uwezo kaamili. Ikiwa hao wamo katika hali hii ya inadi, basi je walio it'ii Haki hawajakata tamaa bado na kuamini kwa hawa makafiri, na wakajua kwamba kufuru yao ni kuyakataa matakwa ya Mwenyezi Mungu? Na lau kuwa Mwenyezi Mungu angeli taka waongoke watu wote basi wangeli ongoka! Na hakika uwezo wa Mwenyezi Mungu uko dhaahiri mbele yao. Basi haziachi balaa kali kali za kuwateketeza zikiwasibu, au kuwateremkia karibu yao, mpaka itimie ahadi ya Mwenyezi Mungu aliyo wapa. Na Mwenyezi Mungu Mtukufu havunji miadi yake.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Allah Mtukufu, Aliyetukuka, Anawarudi makafiri ambao walitaka kwamba Nabii, (rehema za Allah Mtukufu na amani zimshukie), ateremshiwe miujiza yenye kuonekana, kwa kuwaambia, Lau kungekuwa na Qur’ani inayosomwa ikafanya majabali yaondoke mahali pake au ardhi ipasuke itoe mito au wafu wafufuke na waseme, kama walivyotaka kwako, hii Qur’ani ingalikuwa ndiyo yenye kusifika na hayo na si kitu kingine, na pia hawangaliamini. Bali ni ya Allah Mtukufu amri juu ya miujiza na mengineyo. Kwani hawakujua Waumini kwamba lau Allah Mtukufu angetaka, watu wote wa ardhini wangaliamini bila ya miujiza? Na hawataacha makafiri kuendelea kuteremkiwa na mkasa kwa sababu ya ukafiri wao, kama kuuawa na kutekwa katika vita vya Waislamu, au kuteremkiwa na mkasa huo karibu na nyumba zao, mpaka ahadi ya Allah Mtukufu ije ya kuwapa ushindi juu yao. Hakika Allah Mtukufu Haendi kinyume na ahadi Yake.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net