Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 13 · Aya ya 30

Ar-Ra'd 13:30

الرعد

كَذَٰلِكَ أَرْسَلْنَـٰكَ فِىٓ أُمَّةٍ قَدْ خَلَتْ مِن قَبْلِهَآ أُمَمٌ لِّتَتْلُوَا۟ عَلَيْهِمُ ٱلَّذِىٓ أَوْحَيْنَآ إِلَيْكَ وَهُمْ يَكْفُرُونَ بِٱلرَّحْمَـٰنِ ۚ قُلْ هُوَ رَبِّى لَآ إِلَـٰهَ إِلَّا هُوَ عَلَيْهِ تَوَكَّلْتُ وَإِلَيْهِ مَتَابِ

Maana

Ndivyo hivyo tulivyokutuma kwa umma ambao zimekwishapita kabla yao umma nyingine, ili uwasomee yale tuliyokufunulia, na wao wanamkufuru Rahmani (Mwingi wa Rehema)! Sema: Yeye ndiye Mola wangu Mlezi. Hakuna mungu isipokuwa Yeye. Juu yake nimetegemea, na kwake ndiyo marejeo!

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Ndio kama hivi tumekutuma kwa umma ambao wamekwsiha pita kabla yao umati nyengine, ili uwasomee tunayo kufunulia, na wao wanamkufuru Rahmani, Mwingi wa Rehema! Sema: Yeye ndiye Mola wangu Mlezi. Hapana mungu isipo kuwa Yeye. Juu yake nimetegemea, na kwake ndio marejeo yangu! [30]

[30] Kama tulivyo wapelekea kaumu zilizo kwisha pita Mitume wakawaeleza yaliyo ya Haki, na wakapotea walio potea, na wakaongoka walio ongoka, na tukawapa miujiza ya kuonyesha Utume wao, kadhaalika tumekutuma wewe kwa umma wa Kiarabu na wenginewe, na kabla yao zimekwisha pita kaumu nyengine. Na muujiza wako ni hii Qur'ani uwasomee, uwawekee wazi maana yake na utukufu wake. Na wao wanaikanya rehema ya Mwenyezi Mungu walio pewa kwa kuteremshiwa Qur'ani. Basi ewe Nabii! Waambie: Mwenyezi Mungu ndiye aliye niumba, na anaye nilinda, na anaye nirehemu. Hapana mungu wa kuabudiwa kwa Haki ila Yeye. Namtegemea Yeye tu, na kwake ndio marejeo yangu na yenu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Kama tulivyowatuma Mitume kabla yako, tulikutuma, ewe Mtume, katika ummah waliopita kabla yao ummah wa Mitume, ili uwasomee ummah huu Qur’ani iliyoteremshwa kwako, na hali ya watu wako ni kuukanusha upweke wa Mwingi wa rehema. Waambie, ewe Mtume, Mwingi wa rehema Ambaye hamkumpwekesha na kumfanya ni Mola mmoja Ndiye Mola wangu, Peke Yake; hakuna mwenye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Yeye. Kwake Yeye nimetegemea na nina imani, na Kwake Yeye ndio marejeo yangu na makimbilio yangu.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Ar-Ra'd

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net