Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 13 · Aya ya 29

Ar-Ra'd 13:29

الرعد

ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَعَمِلُوا۟ ٱلصَّـٰلِحَـٰتِ طُوبَىٰ لَهُمْ وَحُسْنُ مَـَٔابٍ

Maana

Wale walioamini na wakatenda mema watakuwa na raha na marejeo mazuri.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wale walio amini na wakatenda mema watakuwa na raha na marejeo mazuri. [29]

[29] Na hakika wanao inyenyekea Haki, na wakasimama kutenda vitendo vyema, hao watapata malipo mema, na mwisho mzuri.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Wale waliomuamini Allah Mtukufu na Mtume Wake na wakafanya matendo mema watakuwa na furaha, kitulizo cha jicho, hali nzuri na marejeo mema kwenye Pepo ya Allah Mtukufu na radhi Zake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Ar-Ra'd

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net