Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 13 · Aya ya 28

Ar-Ra'd 13:28

الرعد

ٱلَّذِينَ ءَامَنُوا۟ وَتَطْمَئِنُّ قُلُوبُهُم بِذِكْرِ ٱللَّهِ ۗ أَلَا بِذِكْرِ ٱللَّهِ تَطْمَئِنُّ ٱلْقُلُوبُ

Maana

Wale walioamini na zikatua nyoyo zao kwa kumtaja Mwenyezi Mungu. Sikilizeni! Kwa kumtaja Mwenyezi Mungu ndiyo nyoyo hutua!

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Wale walio amini na zikatua nyoyo zao kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu. Hakika kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu ndio nyoyo hutua! [28]

[28] Na hakika hawa wanao rejea kwa Mwenyezi Mungu, na wanaikubali Haki, ndio hao walio amini ambao nyoyo zao zinatua anapo tajwa na kukumbukwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa Qur'ani au vyenginevyo. Na hakika nyoyo hazitulii na kutua ila kwa kukumbukwa utukufu wa Mwenyezi Mungu na uwezo wake na kuombwa radhi yake kwa kumt'ii.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na Anawaongoza wale ambao nyoyo zao zimetulia kwa kumpwekesha Allah Mtukufu na kumtaja zikapata utulivu. Jua utanabahi kwamba kumtii Allah Mtukufu, kumtaja na malipo mema kutoka Kwake yanafanya nyoyo zitulie.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Ar-Ra'd

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net