Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 13 · Aya ya 27

Ar-Ra'd 13:27

الرعد

وَيَقُولُ ٱلَّذِينَ كَفَرُوا۟ لَوْلَآ أُنزِلَ عَلَيْهِ ءَايَةٌ مِّن رَّبِّهِۦ ۗ قُلْ إِنَّ ٱللَّهَ يُضِلُّ مَن يَشَآءُ وَيَهْدِىٓ إِلَيْهِ مَنْ أَنَابَ

Maana

Na wanasema wale waliokufuru: Kwa nini hakuteremshiwa ishara kutoka kwa Mola wake Mlezi? Sema: Hakika Mwenyezi Mungu humpoteza amtakaye, na humwongoa anayerudi kwake.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Na wanasema walio kufuru: Kwa nini hakuteremshiwa muujiza kutoka kwa Mola wake Mlezi. Sema: Hakika Mwenyezi Mungu humwacha kupotea amtakaye, na humwongoa anaye elekea kwake, [27]

[27] Na hakika hao washirikina walio banwa na wingi wa pupa na papara husema: Je, huyu Nabii hakuteremshiwa muujiza mwengine kutoka kwa Mwenyezi Mungu? Ewe Nabii! Waambie: Sababu ya kutokuwa na Imani nyinyi si upungufu wa miujiza, bali ni upotovu tu! Na Mwenyezi Mungu Aliye takasika na Aliye tukuka humwacha apotee anaye mtaka apotee, maadamu anaendelea katika njia ya upotovu. Na humwongoa aendee kwenye Haki yule ambae daima hurejea kwa Mwenyezi Mungu.

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Na makafiri wanasema kwa kushindana, Si ateremshiwe Muhammad miujiza inayoonekena kama miujiza ya Mûsã na ‛Ǐsã. Waambie kwamba Allah Mtukufu Anampoteza Anayemtaka miongoni mwa washindani wasiotaka uongofu na haimfai miujiza, na Anawaongoza kwenye dini Yake ya haki anayerejea Kwake na kutaka radhi Zake.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Ar-Ra'd

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net