Ruka hadi kwenye maudhui
Sura ya 13 · Aya ya 26

Ar-Ra'd 13:26

الرعد

ٱللَّهُ يَبْسُطُ ٱلرِّزْقَ لِمَن يَشَآءُ وَيَقْدِرُ ۚ وَفَرِحُوا۟ بِٱلْحَيَوٰةِ ٱلدُّنْيَا وَمَا ٱلْحَيَوٰةُ ٱلدُّنْيَا فِى ٱلْـَٔاخِرَةِ إِلَّا مَتَـٰعٌ

Maana

Mwenyezi Mungu humkunjulia riziki amtakaye, na humkunjia kwa kipimo. Na waliufurahia uhai wa dunia. Na uhai wa dunia kwa kulinganisha na Akhera si kitu isipokuwa ni starehe ndogo.

Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com

Maana

Mwenyezi Mungu humkunjulia riziki amtakaye, na humkunjia kwa kipimo. Na wamefurahia maisha ya dunia. Na uhai wa dunia kwa kulingana na Akhera si kitu ila ni starehe ndogo. [26]

[26] Na ikiwa hao washirikina wanaona kuwa wao wamepewa mali mengi, na Waumini ni mafakiri, wanyonge, basi wajue kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu humpa riziki kunjufu amtakaye akizishika sababu na humdhikisha amtakaye. Basi Yeye humpa Muumini na asiye kuwa Muumini. Kwa hivyo msidhani kuwa wingi wa mali mikononi mwao kuwa ni dalili ya kuwa wao ndio wamo katika Haki. Lakini wao hufurahi kwa hayo mali walio pewa, juu ya kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu humpa dunia anaye mpenda na asiye mpenda. Na maisha ya duniani si chochote ila ni starehe duni yenye kupita!

Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com

Maana

Allah Mtukufu Peke Yake Anamkunjulia riziki Anayemtaka miongoni mwa waja Wake na anampunguzia Anayemtaka kati yao. Na makafiri waliufurahia ukunjufu duniani. Na dunia hii haikuwa ikilinganishwa na Akhera isipokuwa ni kitu kidogo cha kustarehe nacho, na kwa haraka sana kinaondoka.

Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com

Ar-Ra'd

Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net