Ar-Ra'd 13:25
الرعدوَٱلَّذِينَ يَنقُضُونَ عَهْدَ ٱللَّهِ مِنۢ بَعْدِ مِيثَـٰقِهِۦ وَيَقْطَعُونَ مَآ أَمَرَ ٱللَّهُ بِهِۦٓ أَن يُوصَلَ وَيُفْسِدُونَ فِى ٱلْأَرْضِ ۙ أُو۟لَـٰٓئِكَ لَهُمُ ٱللَّعْنَةُ وَلَهُمْ سُوٓءُ ٱلدَّارِ
Na wale wanaovunja agano la Mwenyezi Mungu baada ya kulifunga, na wanakata yale aliyoamrisha Mwenyezi Mungu yaungwe, na wanafanya uharibifu katika ardhi, hao wana laana, na wana Nyumba mbaya.
Maana: Swahili Translation - Rowad Translation Center. Issued by the Islamic Content Service Association in Languages Toleo 1.0.5, 2025-12-17. QuranEnc.com
Na wale wanao vunja ahadi ya Mwenyezi Mungu baada ya kuzifunga, na wanakata aliyo amrisha Mwenyezi Mungu yaungwe, na wanafanya fisadi katika nchi: hao ndio watakao pata laana, na watapata Nyumba mbaya. [25]
[25] Hakika sifa za Waumini wema ni kinyume na sifa za washirikina waovu. Kwani washirikina huvunja ahadi ya Mwenyezi Mungu aliyo chukua kwao kwa mujibu wa maumbile na ambayo walijifunga nayo. Kwa hivyo wamekhalifu maumbile yao na akili zao kwa kuabudu mawe yasiyo wafaa wala kuwadhuru. Na wanavunja ahadi zao wanazo fungamana na waja wenzao, tena wanakata makhusiano yao ya mapenzi na watu, na makhusiano yao na Mwenyezi Mungu. Hawazifuati amri zake, wala hawamuabudu Yeye pekee. Na wanafanya uharibifu katika ardhi kwa uvamizi na kufanya uadui na kuvuka mipaka, na kuacha kuitengeneza dunia wakanafiika nayo! Na Mwenyezi Mungu Aliye takasika hapendi uchafuzi na ufisadi.
Maana: Swahili Translation - Ali Mohsin Al-Barwani. Translated by Ali Mohsen Al-Barwani Toleo 1.0.1, 2025-06-25. QuranEnc.com
Ama waovu, wamesifiwa kwa sifa kinyume na zile za Waumini. Wao ni wale ambao hawatekelezi ahadi za Allah Mtukufu kwa kumpwekesha, kutakasika na sifa za upungufu ni Kwake, kwa ibada baada ya kujichukulia ahadi ya mkazo. Na wao ni wale wanaokata kile ambacho Allah Mtukufu amewaamrisha kukiunga kama vile kukata udugu na mengineyo na wanafanya uharibifu katika ardhi kwa kufanya maasia. Hao waliosifiwa kwa sifa hizi mbaya watakalolipata ni kufukuzwa kwenye rehema za Allah Mtukufu na watakuwa na mambo ambayo ni mabaya kwao ya adhabu kali katika Nyumba ya Akhera.
Maana: Swahili Translation - Abdullah Muhammad and Nasser Khamis. Translated by Dr. Abdullah Muhammad Abu Bakr & Shaykh Nasser Khamis Toleo 1.0.1, 2026-03-12. QuranEnc.com
Kiarabu ni maandishi ya Tanzil, bila kubadilishwa. Maana ni matoleo ya wachapishaji wake, bila kubadilishwa; wahakiki wa Sabīl wenyewe bado hawajazikagua. Kiarabu: maandishi ya Uthmani ya Tanzil, toleo la 1.1. Chanzo: tanzil.net